1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON.Makampuni 4600 kuchunguzwa katika sakata ya rushwa ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa mafuta kwa chakula nchini Iraq

10 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEmL

Maelfu ya makampuni miongoni mwa makampuni 4600 yaliyonunua mafuta na kuuza chakula kwa Iraq chini ya mpango wa Umoja wa Mataifa yanafanyiwa uchunguzi juu ya madai ya rushwa na vitendo haramu.

Mchunguzi muhimu juu ya madai hayo amesema kwamba tume ya Umoja wa mataifa juu ya madai ya rushwa ya mpango wa mafuta kwa chakula nchini Iraq, inapanga kufanya uchunguzi kamilifu mnamo mwezi Septemba, juu ya jinsi baadhi ya maofisa wa Umoja wa mataifa na mashirika yake, walivyochukua jukumu la kusimamia mpango huo wa mabilioni ya fedha.

Ripoti nyingine inatarajiwa kutolewa mwezi oktoba juu ya maelfu ya makampuni yaliyopewa kandarasi ya kuuza mafuta au chakula, dawa,na mahitaji mengine.

Mpango wa Umoja wa Mataifa ulianzishwa mwaka 1996 kulainisha athari za vikwazo vya kiuchumi iliyowekewa Iraq baada ya kuivamia Kuwait mwaka 1990.