1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington.George Bush aahidi kumsaka na kumuua Osama bin Laden.

21 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDAM

Rais wa Marekani George W. Bush ameahidi kumsaka na kumuuwa kiongozi wa kundi la Al-Qaida Osama bin Laden na magaidi wengine waliopo hata ikiwa ni kuwasaka katika ardhi ya Pakistan.

Bin Laden inaaminika amejificha kaskazini katika vijiji vya makabila karibu na mpaka wa Afghanistan na Pakistan.

Vikosi vya kijeshi vya Marekani vilipelekwa Afghanistan lakini havikuruhusiwa kufanya operesheni zake nchini Pakistan.

Hata hivyo dhamira ya George Bush yakutaka kufanya operesheni nchini Pakistan, haikukaribishwa na Musharraf ambae alisema kuwa Pakistan haitakaribisha harakati za kupambana na ugaidi za Marekani.