1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington: Umoja wa Mataifa umewajibika kuwa na jukumu imara Iraq ...

19 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CFzt
Umoja wa Mataifa umewajibika kuwa na jukumu imara la ujenzi mpya chini Iraq, na jukumu hilo lazima liwekewe mipaka ya msaada wa kiutu, alisema hiyo jana waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Joschka Fischer. Bw. Fischer akiwa mjini Washington mwa mazungumzo na maafisa wa Marekani wa ngazi ya juu, alisema hashuku jukumu la uongozi la Marekani nchini Iraq lakini wakati umewadia kwa Umoja wa Mataifa kujipatia jukumu kubwa zaidi katika nchi hiyo iliyobomolewa kwa vita. Kuhusu uhusiano kati ya Marekani na Ujerumani, ambao ulidhoofika kwa ubishi wa Ujerumani dhidi ya vita vilivyoongozwa na Marekani nchini iraq, Fischer alisema; "Tulikuwa na matatizo, lakini katika siku za nyuma."