1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Ratco Mladic huenda akakamatwa hivi karibuni na kupelekwa huko The Hague.

10 Juni 2005
https://p.dw.com/p/CF56

Maafisa wa Marekani wanaamini kuwa mtu anayetafutwa sana kwa uhalifu wa kivita Ratco Mladic huenda akapatikana hivi karibuni.

Waziri mdogo wa Marekani anayeshughulikia masuala ya kisiasa Nicholas Burns, amesema kuwa Serbia imeongeza juhudi za kumkamata jenerali huyo wa zamani wa jeshi la Bosnia ambaye ni Mserbia na kumpeleka katika mahakama ya umoja wa mataifa inayowahukumu wahalifu wa vita mjini The Hague.

Bwana Mladic amekuwa akijificha kwa muda wa miaka tisa sasa baada ya kutakiwa na mahakama hiyo ya kimataifa kujibu mashtaka ya kuhusika na mauaji ya halaiki katika vita vya Bosnia mwaka 1992 - 95.

Wakati huo huo , Marekani imeamua kuanza tena kuipa misaada Serbia na Montenegro tangu pale Serbia ilipoweza kuwatoa watuhumiwa kadha wa uhalifu wa kivita katika mahakama hiyo ya kimataifa mjini The Hague.