1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIraq

Iraq na Marekani zaanza mazungumzo ya kuondoa vikosi Iraq

27 Januari 2024

Iraq na Marekani zimefanya duru ya kwanza ya mazungumzo hii leo juu ya mustakabali wa vikosi vya wanajeshi wa Marekani na wengine wa kigeni nchini humo.

https://p.dw.com/p/4bkYC
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al-Sudani
Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed Shia Al-Sudani ameanzisha mazungumzo na Marekani juu ya kuwaondoa wanajeshi wa kigeni nchini humoPicha: Murtadha Al-Sudani/Anadolu Agency/Pool via REUTERS

Ofisi ya Waziri Mkuu Mohamed Shia al-Sudani imesema kwenye taarifa kwamba kiongozi huyo amefungua mazungumzo hayo yanayozikutanisha pande zote mbili ili kwa lengo la kuhitimisha operesheni ya vikosi vya muungano wa kimataifa nchini Iraq.

Baghdadinataraji kwamba majadiliano hayo yataibua mpango wa kupunguza uwepo wa vikosi hivyo, na mshauri wa mambo ya nje wa Sudani, Farhad Alaadin amesema urefu wake utatokana na makubaliano na hatua zitakazokuwa zimefikiwa.

Washington ilisema siku ya Alhamisi kwamba imekubaliana na Baghdad juu ya kuanzishwa kwa "vikundi kazi vya wataalamu wa kijeshi na wataalamu wa ulinzi" kama sehemu ya Tume ya Juu ya Kijeshi iliyoundwa kwa ajili ya mazungumzo na Baghdad.