1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yafuatilia kwa karibu mzozo wa siasa nchini Japan

13 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBQH

Kujiuzulu kwa waziri mkuu wa Japan, Shinzo Abe, huenda kukazusha matatizo kwa Marekani. Utawala wa rais George W Bush unafuatilia kwa karibu kuona kama mzozo wa kisiasa nchini Japan utaathiri ushirikiano wa Japan katika harakati za kijeshi zinazoongozwa na Marekani nchini Afghanistan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani, Sean McCormack, amesema hataki ionekane kana kwamba Marekani inaingilia mambo ya ndani ya Japan lakini akasisitiza matumaini yake kwamba waziri mkuu mpya wa Japan atakuwa mshirika mzuri wa Marekani.

Wadadisi wa kisiasa mjini Washington wana wasiwasi kwamba sera ya chama tawala nchini Japan, Japanese Democratic Party, kuelekea Marekani huenda ikabadilika. Marekani ina wasiwasi kuhusu hatima ya sheria ambayo itarefusha muda kwa Japan iendelee kutoa mafuta kwa ajili ya meli za jeshi la muungano katika bahari ya Hindi.

Sheria hiyo inayomalizika mwezi Novemba mwaka huu inapingwa na chama cha upinzani cha Democratic Party nchini Japan.