1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Korea Kaskazini yaanza tena kutumia mtambo wa nuklea

21 Agosti 2005
https://p.dw.com/p/CEiw

Satalaiti za Marekani zimeripoti kugunduwa ishara kwamba Korea Kaskazini hivi karibuni imeanza tena kuutumia mtambo ambao unaweza kutumiwa kwa ajili ya kuzalisha vitu vya kutengenezea makombora ya nuklea.

Hayo yamebainishwa na repoti iliochapishwa na gazeti la Japani la Asahi Shimbum leo hii.Kwa mujibu wa gazeti hilo satalaiti za upelelezi zimegunduwa mvuke ukitoka kwenye bwela liliounganishwa na jengo ulioko mtambo huo huko Yangon. Likiwakariri maafisa walio karibu na mazungumzo ya nuklea ya nchi sita bila ya kuwataja majina limesema mvuke huo umegunduliwa kabla ya kuanza kwa mazungumzo hayo yenye lengo la kuishawishi Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nuklea na badala yake kupatiwa msaada pamoja na hakikisho la usalama.