1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Hakuna ushahidi wa kifo cha Bin Laden

24 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CD9O

Saudi Arabia nayo imekanusha ripoti ya gazeti la Kifaransa,iliyosema kiongozi wa Al-Qaeda,Osama Bin Laden amefariki dunia.Ubalozi wa Saudi Arabia mjini Washington umesema haujapokea habari za aina hiyo.Siku ya Jumamosi Ufaransa,Marekani na Pakistan zilisema kuwa haziwezi kuthibitisha ripoti ya gazeti la L´Est Republicain.Gazeti hilo likinukulu idara za upelelezi za Saudi Arabia na Ufaransa,lilisema,Bin Laden alifariki dunia mwishoni mwa mwezi wa Agosti nchini Pakistan baada ya kuugua taifodi.Inaaminiwa kuwa Bin Laden,anajificha Pakistan karibu na mpaka wa Afghanistan.