1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush atoa wito kuchukuliwa hatua ya haraka kwa taarifa ya uchunguzi wa kifo cha Hariri.

22 Oktoba 2005
https://p.dw.com/p/CEPY

Rais wa Marekani George W. Bush ametoa wito kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa kulishughulikia kwa haraka suala la uchunguzi wa umoja wa mataifa ambao unawahusisha maafisa wa usalama wa Syria na Lebanon na kuuwawa kwa waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri.

Hariri na watu wengine 20 waliuwawa tarehe 14 mwezi wa Februari mwaka huu kwa mlipuko wa bomu mjini Beirut.

Ripoti ya umoja wa mataifa imesema kuwa uamuzi wa kumuua Hariri haungeweza kuchukuliwa bila ya kuidhinishwa kutoka kwa maafisa wa ngazi ya juu wa usalama ambao wameshirikiana na wenzao nchini Lebanon.

Akizungumza katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari pamoja na waziri wa mambo ya kigeni wa Uingereza Jack Straw mjini Birmingham , Alabama , waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amesema kuwa Syria inapaswa kubeba dhamana ya kifo hicho.

Syria imekataa ripoti hiyo ya umoja wa mataifa , ambayo imekabidhiwa na mchunguzi kutoka Ujerumani Detlev Mehlis kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa siku ya Alhamis iliyopita na kuyaita matokeo ya uchunguzi huo kuwa yameingiza athari za kisiasa.