1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Bush ataka kikosi kuwekwa haraka Lebanon

22 Agosti 2006
https://p.dw.com/p/CDJH

Rais George W. Bush wa Marekani ametowa wito wa kuwekwa kwa haraka kikosi cha kimataifa nchini Lebanon kusimamia usitishaji wa mapigano kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hizbollah.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Bush amesema kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa kitasaidia kuizuwiya Hizbollah kuwa taifa ndani ya taifa.Pia amesema serikali yake inaahidi kutowa dola za ziada milioni 230 kuwasaidia Walebanon kuzijenga upya nyumba zao na kurudi kwenye miji na jamii zao.

Kansela Angela Merkel wa Ujerumani pia amesema kikosi hicho cha kimataifa hakina budi kuwekwa kusini mwa Lebanon haraka iwezekanavyo kulinda usitishaji wa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.