1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Bush aahidi kumkamata Bin Laden.

12 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDDC

Miaka mitano baada ya shambulio la kigaidi katika historia ya Marekani , rais George W. Bush amesema jana usiku kuwa vita dhidi ya ugaidi ni kazi ya kizazi chetu na kuwataka Wamarekani kuweka tofauti zao kando na kupambana hadi kupata ushindi.

Bush amesema kuwa Marekani haikutaka vita hivi, na kila Mmarekani anaomba vimalizike.

Vita hivi bado havijamalizika na havitamalizika hadi pale sisi ama magaidi wanashinda. Bush katika hotuba yake ametetea vita dhidi ya Iraq licha ya kuungama kuwa Saddam Hussein hakuhusika na shambulio la septemba 11 ambapo watu karibu 3,000 wameuwawa.

Amesema kuwa utawala wa rais Saddam Hussein licha ya kutokuwa na silaha za maangamizi lakini ulikuwa ni kitisho ambacho dunia haingeweza kuridhia.

Wakati huo huo katika hotuba hiyo ameapa kuwa Marekani itamkamata kiongozi wa mtandao wa kigaidi Osama bin Laden.