1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Watu 12 wauawa katika mashambulizi manne Nigeria

4 Aprili 2023

Watu wapatao 12 wameuliwa na wengine kadhaa kujeruhiwa au kutekwa nyara katika mkururo wa mashambulizi kaskazini mashariki na katikati mwa Nigeria

https://p.dw.com/p/4Pg3u
Nigeria I Ausbruch Hochsicherheitsgefängnis in Kuje
Picha: Afolabi Sotunde/REUTERS

Msemaji wa polisi katika jimbo la Adamawa kaskazini mashariki mwa Nigeria Suleiman Nguroge amesema hapo jana kwamba watu wasiojulikana waliokuwa wamejihami na bunduki walikivamia kijiji cha Dabna katika wilaya ya Hong na kuwaua watu watatu. Nguroge aidha amesema baadhi ya makazi yamechomwa moto.

Hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na hujuma hizo. Katika tukio lingine la jana watu waliokuwa wamejihami na bunduki walizivamia jamii katika mji wa Oganenigu wilaya ya Dekina katika jimbo la  Kogi katikati mwa Nigeria.

Msemaji wa gavana wa jimbo hilo amesema mwanasiasa mmoja wa eneo hilo aliuliwa na wengine wakajeruhiwa katika uvamizi huo.