1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW.Poland kuchangia wanajeshi 1000 katika kikosi cha NATO

14 Septemba 2006
https://p.dw.com/p/CDCP

Poland imetangaza kuwa itawapeleka wanajeshi wake 1000 nchini Afghanistan kujiunga na jeshi la shirika la kujihami la magharibi NATO.

Hatua huyo imefuatia baada ya makamanda wa NATO kutoa mwito wa kuongezwa askari 2500 ili kufanikisha zoezi la kupambana na wanamgambo wa Taliban.

Wanajeshi hao kutoka Poland wanatarajiwa kuwasili nchini Afghanistan mwezi februari mwaka ujao.

Wakati huo huo Ukarain imesema kuwa itasimamisha mpango wake wa kuwapeleka wanajeshi wake katika jeshi la shirika la kujihami la magharibi NATO.

Hayo ni kwa mujibu wa waziri mkuu wa Ukrain Viktor Yanukovich ambae yuko ziarani nchini Ubelgiji.