Warepublican wavuruga kikao cha kumchunguza Trump
24 Oktoba 2019Wabunge wa chama cha Republican, ambao wanashawishiwa na Rais Donald Trump kuchukua hatua kali kukabiliana na jitihada za chama cha Democratic za kumtia hatiani kiongozi huyo kwa tuhuma za kwenda kinyume na maadili ya ofisi yake, jana walivamia kikao kinachochunguza tuhuma hizo dhidi ya Trump kilichokuwa na usalama wa hali ya juu na kuchelewesha mchakato wa utoaji ushahidi. "Nimejumuika hapa pamoja na wabunge wenzangu wengi, chini ya jengo hili. Ili endapo wale waliopo nyuma ya milango ile watajaribu kubadili matokeo ya uchaguzi wa Marekani, tutataka kujua kipi kinachoendelea" Ni Matt Gaetz mwakilishi wa Rebublican kabla ya wabunge wa chama hicho kuvamia.
Alikuwa miongoni mwa zaidi ya wabunge 25 wa chama cha Republican ambao hawakuwa na ridhaa ya kuingia katika ofisi hizo, kusikiliza shauri kuhusu Trump, waliingia ghafla katika chumba ambacho afisa wa ulinzi wa Marekani, anaeshughulikia masuala ya Ukraine na Urusi, Laura Cooper, akijiandaa kutoa ushahidi wake mbele ya wabunge wa Repulican na Demokratic. Wabunge haowalikuwa wakipinga kile walichodai, wapinzani wao chama cha Demokrat, ndio walikuwa wakiongoza uchunguzi huo uliokuwa ukiendeshwa kwa siri.
Wabunge wakiuka kanuni za bunge
Wabunge wao walikiuka, kanuni kwa kuingia na simu. Ikiwa kiusalama ipo wazi kabisa kuwa ni marufuku kuingia na vifaa vya kieletroniki.
Lakini baada ya kuchelewa kwa masaa kadhaa, Cooper alianza kutoa ushuhidi wake. Mzozo huo wa makabiliano, ulionekana kuongeza katika nyakati za uchunguzi, unatishia zaidi urais wa Tramp, na hasa katika kipindi hiki ambacho anataka kuwania tena muhula wake wa pili madarakani hapo mwakani. Wabunge waRepublican wamesababisha mkwamo kwa kamati tatu za bunge zinaongozwa na Wademocratic, katika kuchunguza kabla kuamua kuondoka katika chumba cha kusikilizia shauri.
Uchunguzi wa kumshitaki rais Trump unazingatia, maombi ya kiongozi huyo kwa Ukraine, kumchunguza hasimu wake wa ndani Mdemokrat- Joe Biden kwa kujinufaisha kisiasa. Kwa hivyo kwa kitendo hicho cha wabunge ambao ni wafuwasi wake kuvamia katika chumba cha kusikilizia shauri, kunanonekana kama ni fikra ya washirika wa Trump kuonesha kwamba jambo linalofanyika kuwa ni mbinu ya kisiasa isiyo ya haki, na si tabia isio ya uadilifu ya rais kama inavyoelezwa.
Mbunge Leader Kevin McCarthy aliwambia waandishi wa habari kwamba raia wa Marekani wana sauti katika mchakato huo. Wana haki ya kujua. Lazima jambo hilo lifanyike kwa uwazi. Ingawa wabunge wa Repulican wanalalamikia ukosefu wa uwazi katika uchunguzi huo, lakini katiba inalipa bunge mamlaka ya kuandaa mchakato wa mashitaka na kuandaa kanuni za uchunguzi. Uchunguzi unafanyika katika chumba cha siri ambacho kimeandaliwa kwa namna ya kuwapa wabunge taarifa za siri au nyaraka nyeti.