1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kwanini wahindi wanapinga mpango mpya wa kuajiri wanajeshi?

23 Juni 2022

Maeneo makubwa katika nchi ya India yamekumbwa na maandamano, ya kupinga sera mpya ya serikali ya kuajiri wanajeshi.

https://p.dw.com/p/4D6fZ
Indien Protesten in Bengal
Picha: Satyajit Shaw/DW

Mnamo juni 14, waziri mkuu wa India Narendra Modi  alizindua mpango uitwao Agnipath, au "njia ya moto," mpango maalum ulionzishwa wa kuajiri watu zaidi jeshini kwa mkataba wa miaka minne na kupunguza umri wa wastani wa wanajeshi milioni 1.38 nchini India.mpango huo kimsingi lengo lake ni kuliimarisha jeshi la ulinzi na kuliweka katika viwango vya kisasa.

Chini ya sera ya Agnipath, takriban watu  46,000 wataandikishwa kwenye mafunzo ya kijeshi mwaka huu, na asilimia 25 tu ndio watakaobakia mpaka mwisho wa mkataba wao wa miaka minne.  Makuruta hao  watapitia mafunzo kwa miezi sita na kisha watatumikia  jeshini  kwa miaka mitatu na nusu.

Kwanini sera ya Agnipath?

Maafisa wakuu wa ulinzi wanasema mpango huo ni mageuzi yanayotekelezwa ili kurekebisha miundombinu ya usalama na kupunguza gharama za mishahara na pensheni, ambayo ni nusu ya bajeti ya ulinzi ya India, kwani inachangia zaidi ya dola bilioni 75.

Indien | Proteste gegen Armee-Rekrutierungsprogramm Agnipath
Maandamano dhidi ya usajili wa wanajeshi wapyaPicha: ANI/Handout/REUTERS

Ajai Shukla, kanali mstaafu na mchambuzi wa masuala ya ulinzi, aliiambia DW kuwa "Serikali haikuwa na chaguo zaidi ya  kutekeleza mpango wa Agnipath,  kwa sababu imezingatia gharama kubwa ya wafanyakazi wa kijeshi, ambayo iliacha pesa kidogo kwa ajili ya kuboresha vifaa. Aliongezea kuwa "Ingawa pia kutakuwa na faida kama vile kupunguza umri wa wastani wa jeshi, faida kuu ni kwamba wanajeshi wanaostaafu baada ya miaka minne hawatalazimika kulipwa pensheni,".

SK Chatterji, Brigedia mstaafu anayeunga mkono mpango huo, aliiambia DW kwamba inaendana na taratibu za kuajiri wanajeshi duniani kote."Itapunguza wastani wa umri kutoka miaka 32 hadi 26 na kuwapa vijana fursa ya kuitumikia nchi. Lakini, muhimu zaidi, itaokoa bajeti ya pensheni na kuruhusu bajeti zaidi ya maboresho ya vifaa ,".

Chatterji aliongezea, kutakuwa na nafasi ya  asilimia 75 ya ajira ya wanajeshi ambao watalazimika kuondoka jeshini kufuatia muda wao wa miaka minne.

Soma zaidiUjerumani na India zatiliana saini mkataba wa maendeleo

Kwanini Vijana wengi wanapinga mpango huo?

Mpango huo umezua maandamano ya ghasia katika baadhi ya maeneo ya nchi, huku maelfu ya vijana wakishambulia mabehewa ya treni, kuchoma  moto matairi, kuharibu mali ya umma na kushambulia nyumba za viongozi wa kisiasa.Vijana wanataka mpango huo ufutwe.

Wizara ya Reli imesema zaidi ya treni 500 zimesitishwa safari zake  jumatatu kwa sababu ya maandamano hayo.

Indien Protesten in Bengal
Maandamano ya kupinga Agnipath IndiaPicha: Satyajit Shaw/DW

Viongozi wa chama cha upinzani cha Congress wamekutana na Rais wa India Ram Nath Kovind ili kutaka kuondoa mpango huo.

Moja ya wasiwasi mkubwa ni hatima ya wanajeshi hao baada ya kumaliza muda wao.Waandamanaji hao wanasema mpango huo utawanyima fursa ya kazi ya kudumu katika jeshi, pensheni ya uhakika, pamoja na  hadhi ya kijamii.

"Tunajiandaa kwa miaka mingi kuwa wanajeshi katika jeshi kwani inaleta heshima na kipato kwa wakati. Tunawezaje kutegemea mpango huo ambao hakuna uhakika wa maisha yetu ya baadaye na familia?" Pradeep Lal, muandamanaji kutoka jimbo la Haryana, aliiambia DW.

Manoj Pandey, mgombea kutoka Bihar, aliiambia DW kuwa  "hakukuwa na usajili ndani ya jeshi kwa miaka miwili iliyopita kwa sababu ya janga la Corona h. Kuna maanai gani ya kuwa na mpango kama huo?" Pandey aliiambia DW.

Pandey aliongezea kuwa,"Tunawezaje kujitolea kwa jeshi wakati hakuna msaada wa kifedha  baada ya muda mfupi kama huo?"