1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaArgentina

Argentina yafanya uchaguzi katikati ya mdororo wa kiuchumi

19 Novemba 2023

Argentina inafanya duru ya pili ya uchaguzi huku taifa hilo likiwa na shauku ya kupata kiongozi atakayesaidia kulinusuru kutoka kwenye uchumi uliodorora.

https://p.dw.com/p/4Z926
Buenos Aires | Duru ya pili ya uchagzi wa rais
Raia wa Argentina akipiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais mjini Buenos Aires, Novemba 19, 2023Picha: AGUSTIN MARCARIAN/REUTERS

Uchaguzi huo aidha unakabiliwa na kinyang'anyiro kikali kati ya Waziri wa Uchumi Sergio Massa na mwanauchumi Javier Milei.

Wagombea hao wawili wana mitizamo tofauti juu ya mustakabali wa uchumi wa taifa hilo la tatu kwa ukubwa barani Amerika ya Kusini, unaokabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei, kufuatia madeni ya muda mrefu, usimamizi mbaya wa fedha na kuyumba kwa sarafu.

Kura zilianza kupigwa majira ya saa 2:00 asubuhi kwa saa za nchini humo na zitafungwa saa 12:00 jioni, huku matokeo yakitarajiwa muda mfupi baada ya kufungwa kwa vituo.

Massa, 51, ni mwanasiasa mwenye haiba na mzoefu anayetaka kuwashawishi Waajentina kumwamini licha ya utendaji wake kama waziri wa uchumi ulioshuhudia mfumuko wa bei wa kila mwaka ukifikia asilimia 143 na rekodi ya juu ya viwango vya umaskini.

Mpinzani wake ameahidi pamoja na mambo mengine kusitisha matumizi yasiyodhibitiwa ya Argentina