1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Wapiganaji wa kundi la Wagner wajiandaa kuondoka Bakhmut

22 Mei 2023

Kiongozi wa kundi la wapiganaji binafsi la Wagner,Yevegeny Prigozhin amesema wapiganaji wake wataondoka kwenye mji wa Bakhmut mashariki mwa Ukraine Juni Mosi.

https://p.dw.com/p/4Resa
Kämpfe und Zerstörung in Bachmut, Ukraine
Picha: UKRAINIAN ARMED FORCES/REUTERS

Kiongozi huyo wa Wagner amesema watakukabidhi majukumu kwa jeshi la Urusi, baada ya kundi hilo kudai limeudhibiti kikamilifu mji huo. Wapiganaji hao pamoja na jeshi la Urusi wote wamesema mji wa Bakhmut uko mikononi mwao, ingawa serikali ya Ukraine mjini Kiev imekanusha madai hayo ikisema bado wanajeshi wake wako kwenye mji huo na mapambano yanaendelea.

Kiongozi wa kundi la Wagner amesema wapiganaji wake wamekwishaweka  eneo la ulinzi katika vitongoji kadhaa katika eneo la Magharibi mwa mji huo kabla ya mpango huo wa kukabidhi majukumu kwa jeshi la Urusi.

Soma pia: Kundi la Wagner ladai kuudhibiti mji wa Bakhmut

Hatua ya kuondoka wapiganaji hao kwa mujibu wa Prighozin itaanza Mei 25 mpaka Juni Mosi. Rais Vladimir Putin amelipongeza kundi hilo la Wagner na wanajeshi wa nchi yake kufuatia madai ya  ushindi huo.