1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Watu wa Thuringia na Saxony washiriki uchaguzi muhimu

1 Septemba 2024

Wapiga kura katika majimbo ya Ujerumani ya Thuringia na Saxony wanafanya uchaguzi wa mabunge ya majimbo ambao unaweza kuinua usawa wa mamlaka katika majimbo yote mawili na kusababishwa athari ya mwelekeo huo kwa taifa.

https://p.dw.com/p/4k9C3
Uchaguzi wa Jimbo la Thuringia - kituo cha kupigia kura
Uchaguzi wa Jimbo la Thuringia - kituo cha kupigia kuraPicha: Martin Schutt/dpa/picture alliance

Kura za maoni za kabla ya uchaguzi huu wa leo zimekiweka chama cha siasa kali za mrengo wa kulia cha Alternative for Germany, AfD kwenye nafasi ya ushindi wa wazi katika jimbo la Thuringia na kwa nafasi ndogo sana wakiwa nyuma ya chama cha siasa za wastani za mrengo wa kulia Christian Democrats (CDU) huko Saxony.

Matokeo ya uchaguzi huo wa leo yataamua uwiano wa mamlaka katika jimbo mabunge ya Thuringia na Saxony, ambayo kila moja lina nafasi kubwa ya kuhodhi nguvu za kisiasa katika masuala ya kikanda.