1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMamlaka ya Palestina

Wapalestina wakalia kiti cha "Dola ya Palestina" ndani ya UM

11 Septemba 2024

Wapalestina wamekalia kwa mara ya kwanza kiti miongoni mwa mataifa wanachama Umoja wa Mataifa katika siku ya kwanza ya mkutano wa kila mwaka wa Baraza Kuu la umoja huo uliofunguliwa jana mjini New York.

https://p.dw.com/p/4kU3A
Kiti kinachowakilisha haki ya uanachama wa Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa
Kiti kinachowakilisha haki ya uanachama wa Palestina ndani ya Umoja wa Mataifa.Picha: Justin Lane/epa/dpa/picture alliance

Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Riyad Mansour aliketi kwenye kiti ndani ya ukumbi wa mikutano kilichoandikwa "Dola ya Palestina" ambacho kimewekwa katikati ya mataifa mawili ya Sri Lanka na Sudan.

Hatua hiyo inafuatia kura iliyopigwa na Baraza Kuu mnamo mwezi Mei ambapo idadi kubwa ya nchi wanachama ziliridhia Palestina itambuliwe kuwa mwanachama kamili wa Umoja wa Mataifa.

Hata hivyo uamuzi huo ulizuiwa kwa kura ya turufu ya Marekani ulipofikishwa mbele  Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Licha ya hayo, azimio hilo la mwezi Mei limetoa haki zaidi kwa ujumbe wa Wapalestina kwenye Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na kupata kiti ndani ya ukumbi wa mikutano lakini bila kuwa na haki ya kupiga kura.