Migogoro katika jimbo la Marsabit nchini kenya imekuwa ikihushuhudiwa kwa miongoo kadhaa sasa na mara nyingi,wanaume wamekuwa wakilaumiwa kuendeleza hali hii ambayo imepelekea mamia ya watu kuuawa kila machafuko ya kikabila yanapozuka. Makala ya wanawake na Maendeleo yanamulika juhudi za wanawake kutoka jimbo la Marsabit ambao wamejitolea kuhakikisha amani inadumu na vita vinakoma.