1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanasiasa wa upinzani Tanzania wamsifu rais Samia

Florence Majani4 Januari 2023

Siku moja baada ya Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania kuondoa marufuku ya mikutano ya hadhara iliyowekwa na mtangulizi wake, Hayati John Magufuli, kwa vyama vya upinzani na kuukwamua mchakato wa katiba mpya, baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa nchini humo wanasema ni tukio la kihistoria.

https://p.dw.com/p/4LjuD

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari mchana wa leo, viongozi  hao wamesema hilo ni tukio la kwanza katika historia ya Tanzania, tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Rais Samia amepongezwa kwa hatua hiyo ya kuruhusu mikutano ya hadhara iliyozuiwa mwaka 2016  na hayati Rais John Magufuli aliyetumia hoja kwamba wananchi walihitaji muda wa kufanya kazi na hivyo vyama vilipaswa kusubiri hadi wakati wa uchaguzi wa 2020.

Kwa upande wake, Kiongozi wa chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Selasini, alipongeza hatua ya Rais Samia, lakini akatoa angalizo kuwa, huenda wapo aliowaita wahafidhina ambao hawajapendezwa na maamuzi ya Rais:

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamemsifu Rais Samia kwa kuwarudisha Chadema katika ushiriki wa matukio ya kisiasa, yanayoandaliwa na serikali, hatua waliyoeleza kuwa ni ukomavu wa kisiasa. 

Hata hivyo, mkutano huu wa waandishi wa habari na vyama vya siasa haukuhudhuriwa na chama hicho kikuu cha upinzani, CHADEMA: