1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo waua watu 15 katika shambulio mashariki mwa Kongo

29 Agosti 2023

Watu 14 wameuawa katika shambulio la wanamgambo lililotokea katika kijiji kimoja cha Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://p.dw.com/p/4VhIM
Vurugu zimekuwa zikiongezeka mashariki mwa Kongo, ambako migogoro imedumu kwa miongo kadhaa.
Vurugu zimekuwa zikiongezeka mashariki mwa Kongo, ambako migogoro imedumu kwa miongo kadhaa.Picha: ALEXIS HUGUET/AFP

Jeshi la Kongo limesema wapiganaji kutoka kundi la CODECO, walifanya mashambulio katika kijiji cha Gobu Jumapili jioni na kuwaua raia 9 na askari mmoja.

Wapiganaji wanne walifariki katika mapigano hayo. Askari wawili na raia wawili walijeruhiwa.

Vurugu zimekuwa zikiongezeka mashariki mwa Kongo, ambako migogoro imedumu kwa miongo kadhaa.

Zaidi ya makundi 120 yenye silaha yanapigana katika eneo hilo, mengi yakiwania ardhi na udhibiti wa migodi yenye madini ya thamani.

CODECO ni kundi la wanamgambo kutoka kabila la Lendu, na tangu mwaka 2017 limekuwa likipigana na kundi la Zaire, kutoka kabila la Hema.