1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Hezbollah wa Lebanon wafyetuwa maroketi kuelekea Israel

5 Julai 2024

Wanamgambo wa Hezbollah nchini Lebanon wamefyetuwa zaidi ya maroketi 200 na droni kadhaa kuelekea ngome za wanajeshi wa Israel jana Alhamisi.

https://p.dw.com/p/4huDU
Israel I Mashambulizi ya roketi na droni
Israel na Hezbollah wamekuwa wakifyatuliana maroketi na droni katikati ya mzozo unaozidi kuongezeka katika eneo la mpakani baina ya pande hizoPicha: Ayal Margolin/REUTERS

Hatua ambayo inaongeza wasiwasi wa mvutano huo kutanuka kati ya kundi hilo na Israel.

Hezbollah imesema mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya jeshi Kaskazini mwa Israel katika milima ya Golan kulipiza kisasi cha kuuliwa mmoja wa makamanda wake kufuatia shambulizi lililofanywa na  Israel.

Mashambulizi ya Hezbollah dhidi ya Israel yameongezeka wakati Israel ikiendelea kuwa vitani na kundi la Hamas katika Ukanda wa Gaza baada ya miezi kadhaa ya mkwamo wa juhudi za kutafuta usitishwaji mapigano katika eneo hilo.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekubali kupeleka ujumbe kwenye mazungumzo yanayolenga kufanikisha hatua ya kuachiliwa huru mateka wanaoshikiliwa na kundi la Hamas tangu shambulio la Oktoba 7.

Chanzo kinachofahamu kinachoendelea kwenye mazungumzo ya Doha,kimeeleza kwamba ujumbe huo wa Israel unaoongozwa na mkuu wa shirika la Ujasusi la Israel David Barnea umeelekea Doha kwa mazungumzo na waziri mkuu wa Qatar.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW