1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanamgambo 40 wa Taliban wauawa

3 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CVtD

KABUL.Majeshi ya Afghanistan na yale ya NATO yamefanikiwa kuwanua wanamgambo wa 40 wa kitaliban huko kusini wa nchi hiyo.

Majeshi hayo yalipambana na wanamgambo hao katika milima kwenye jimbo la Kandahari ambapo wanamgambo 10 walitekwa.

Katika nchi jirani ya Pakistan watu sita wameuawa baada ya kombora lililofyatuliwa na mzinga wa majeshi ya serikali kutua katika makazi ya raia.

Maafisa wa Pakistan wanasema kuwa nyumba mbili katika jimbo lenye ghasia la Waziristan zilipigwa na kombora hilo.

Jimbo hilo la Waziristan lililoko kaskazini mwa Pakistan inaaminika ni maficho ya wapiganaji wa Al Qaida na Taliban kutoka Afghanistan.