1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi zaidi wa Mali wauawa

3 Agosti 2020

Jeshi la Mali limepata pigo tena baada ya mashambulizi mawili kusababisha vifo vya wanajeshi watano wakati ambapo nchi hiyo ya ukanda wa Sahel inakabiliwa na mzozo wa kisiasa unaoipa wasiwasi jamii ya kimataifa.

https://p.dw.com/p/3gKYW
Mali I Symbolbild I Lage in Diabaly
Picha: Getty Images/AFP/P. Guyot

Duru kutoka jeshi zinasema wanajeshi wengine watano wamejeruhiwa baada ya uvamizi katika msafara wa kijeshi na shambulizi katika kambi huku mashambulizi yote yakidaiwa kufanywa na wapiganaji wa jihadi katika eneo la kati la Mali.

Umwagaji huu wa damu unatokea wiki sita baada ya wapiganaji hao kuuvamia msafara wa kijeshi na kuwauwa wanajeshi 24.

Makundi ya kijihadi yalianzisha mashambulizi kaskazini mwa Mali mwaka 2012 na kutokea wakati huo mashambulizi hayo yameenea hadi katikati mwa nchi hiyo na katika nchi jirani za Burkina Faso na Niger, licha ya uwepo wa maelfu ya wanajeshi wa kulinda amani wa Ufaransa na Umoja wa Mataifa.