1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi watano wa Mali wauawa

19 Septemba 2023

Wanajeshi watano wa Mali wameuawa baada ya shambulizi kutokea kwenye kambi mbili za kijeshi siku ya Jumapili.

https://p.dw.com/p/4WYtn
Symbolbild Mali Islamistischer Terrorismus
Picha: Baba Ahmed/AP/dpa/picture alliance

Vuguvugu la Ukombozi la Azawad (CMA) linalojumuisha makundi ya waasi wa Tuareg, limedai kuhusika katika shambulizi hilo.

Wanajeshi wengine 11 hawajulikani walipo.

Jeshi limesema kwamba pia ndege yake imeharibiwa wakati wa mapigano kwenye mji wa Lere, katika jimbo la Timbuktu, kaskazini mwa Mali.

Soma zaidi: Waasi wa Azawad watangaza vita na utawala wa kijeshi Mali

Kundi hilo pia limesema limechukua udhibiti wa kambi mbili za kijeshi huko Lere na kuidungua ndege ya kijeshi.

Kwa mujibu wa maelezo yanayokinzana kutoka pande hizo mbili, washambuliaji waliondoka au walifukuzwa kutoka kwenye eneo hilo na jeshi la ardhiini likisaidiwa na kikosi cha anga.

Hilo ni shambulizi la hivi akribuni dhidi ya kambi ya jeshi kaskazini mwa Mali, ambalo katika wiki za hivi karibuni limeshuhudia kuzuka tena kwa mashambulizi ya waasi wanaotaka kujitenga au wapiganaji wa jihadi.