1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi wa Urusi wasonga mbele kaskazini mashariki Ukraine

7 Agosti 2023

Vikosi vya Urusi vimesonga mbele kiasi kilomita tatu kwenye uwanja wa vita kaskazini mashariki mwa Ukraine katika wakati vinajaribu kurejesha udhibiti wa maeneo viliyoyapoteza mwanzoni kabisa mwa uvamizi wake.

https://p.dw.com/p/4Us4H
Ukraine, Cherson | Schäden an der Genichesk Brücke
Picha: Acting Kherson Region Governor/TASS/IMAGO

Wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema katika muda wa siku tatu zilizopita vikosi vyake vimeingia umbali wa kilometa tatu upande wa adui katika mji wa  Kupiansk ulio kitovu cha mapigano katika wiki za karibuni. 

Soma zaidi: Mkutano wa kimataifa juu ya Ukraine wamalizika Jeddah

Mji huo na maeneo yanayouzunguza mkoa wa Kharkiv vilikombolewa na vikosi vya Ukraine mnamo Septemba mwaka jana, lakini tangu wakati huo Moscow imekuwa ikijaribu kuukamata tena. 

Hayo yanajiri wakati pande hizo mbili zimeshambuliana kwa makombora na ndege zisizo na rubani mwishoni mwa juma. Urusi imeulemga mji mkuu Kyiv usiku wa kuamkia leo huku Ukraine imeilenga miundombinu mkwenye maeneo yaliyonyakuliwa na Moscow.