1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaCanada

Marekani na Canada wadungua kifaa kinachotia mashaka

12 Februari 2023

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau amefahamisha jana kuwa wanajeshi wa nchi yake kwa ushirikiano na wale Marekani wamefanikiwa kudungua kifaa ambacho hadi sasa hakijafahamika vyema na ambacho kilikiuka anga ya Canada.

https://p.dw.com/p/4NNqN
U.S. Air Force F-22 Raptor
Picha: Airman 1st Class Mikaela Smith/U.S. Air Force/UPI Photo /Newscom/picture alliance

Kifaa hicho kilidunguliwa kaskazini-magharibi mwa Canada huko Yukon na ndege ya Marekani chapa F-22, na kimekuwa kifaa cha tatu kudunguliwa na Marekani katika muda wa wiki moja.

Wanajeshi wa Marekani  waliharibu puto la China wikendi iliyopita na baadaye kudungua kifaa chengine huko Alaska.

Washington imekuwa ikiishutumu Beijing  kutumia vifaa hivyo kwa ajili ya ujasusi, shutuma zinazokanushwa na China ambayo inasema puto hilo lilikuwa na madhumuni ya kiraia hasa katika masuala ya utabiri wa hali ya hewa.