1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Wanajeshi 6 wa Nigeria waliokuwa katika doria Benin wauwawa

17 Juni 2024

Jeshi la Niger limesema wanajeshi sita waliokuwa wanalinda bomba la mafuta kwa nchi jirani ya Benin wameuwawa katika shambulizi linalodaiwa kutekelezwa na makundi ya wahalifu waliojihami kusini mwa taifa hilo.

https://p.dw.com/p/4h8f0
Maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Niger wakiwa katika mazungumzo.
Maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Niger wakiwa katika mazungumzoPicha: Balima Boureima/picture alliance/AA

Shambulizi hilo limetokea katika mji wa nje kidogo wa Salkam. Hili lilikuwa shambulizi la kwanza dhidi ya bomba hilo la mafuta lililo kilomita 2000 linalounganisha  eneo la mafuta la kaskazini Mashariki la Agadem na bandari ya Benin ya Seme Kpodji

Soma pia:Mzozo wa Benin-Niger waongezeka baada ya raia wa Niger kuzuiwa Benin

Jeshi hilo limesema limefanikiwa kulifurusha kundi hilo na pia kuwakamata baadhi ya wanachama wake waliojeruhiwa.