1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Wanajeshi Israel wamuua kwa risasi mwanaume wa Kipalestina

30 Januari 2023

Wanajeshi wa Israel wamempiga risasi na kumuua mwanaume mmoja wa Kipalestina huko Ukingo wa Magharibi katika kisa kingine cha wimbi la umwagaji wa damu linalotishia kuongeza mvutano kati ya Israel na Palestina.

https://p.dw.com/p/4MrWk
Israel | Nach Anschlag in Jerusalem
Picha: Mostafa Alkharouf/AA/picture alliance

Wizara ya Afya ya Palestina imesema mwanaume huyo aliyetambuliwa kwa jina la Nassim Abu Fouda alipigwa risasi mjini Hebron, eneo ambalo limekuwa kitovu cha mapambano kati ya jeshi la Israel na Wapalestina.

Soma pia:Mashambulizi yatishia kuzusha mapigano mapya Mashariki ya Kati

Ghasia kati ya Israel na Palestina zimeongezekasiku za karibuni, baada ya uvamizi wa jeshi la Israel kusababisha vifo vya watu 10 na wiki iliyopita na baadaye mshambuliaji wa kipalestina kuwaua raia 7 wa Israel mjini Jerusalem.