1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Wanajeshi 63 wa Urusi wauawa, Ukraine

2 Januari 2023

Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi wake 63 waliuawa mashariki mwa Ukraine wakati vikosi vya Ukraine viliposhambulia kambi yao.

https://p.dw.com/p/4LeJX
Krim Simferopol, russische Soldaten
Picha: Filippo Monteforte/AFP/Getty Images

Wizara ya ulinzi ya Urusi imeeleza kuwa watatoa msaada kwa jamaa wa wanajeshi waliopoteza maisha yao.

Hata hivyo bila ya kudai kuhusika na shambulio hilo, jeshi la Ukraine limesema idadi ya watu waliofariki kutokana na shambulio hilo katika mji wa Makiivka katika eneo linalodhibitiwa na Moscow katika upande wa mashariki mwa Donetsk, ilikuwa kubwa zaidi tofauti na iliotajwa na Urusi.

Urusi haikueleza sehemu kulikotokea shambulio hilo, lakini vikosi vya Ukraine vinaaminika kufanya shambulio wakati wanajeshi wa Urusi walipokuwa wanasherehekea mkesha wa mwaka mpya.

Taarifa ya vifo hivyo 63 ni tangazo la nadra sana la Urusi katika vita vyake nchini Ukraine.