1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 4 wa Pakistan wauawa katika shambulio la mpakani

1 Aprili 2023

Wanajeshi 4 wa Pakistan wameuawa katika shambulio la kuvuuka mpaka kutokea Iran. Taarifa ya jeshi la Pakistan imesema kuwa kundi la magaidi wanaoendesha shughuli zao kutoka upande wa Iran walishambulia walinzi wa doria.

https://p.dw.com/p/4Pagb
Pakistan | Anschlag auf Polizeifahrzeug
Picha: Mohammad Aslam/AFP/Getty Images

Wanajeshi wanne wa Pakistan wameuawa katika shambulio la kuvuuka mpaka kutokea Iran. Taarifa ya jeshi la Pakistan imesema kuwa kundi la magaidi wanaoendesha shughuli zao kutoka upande wa Iran walishambulia walinzi wa doria kwenye mpaka wake na Iran katika wilaya ya Balochistan. Pakistan na Iran zina mpaka wa pamoja wa zaidi ya kilomita 900 na kumekuwa na matukio kadhaa ya mashambulizi kipindi cha nyuma.

Mkoa wa Balochistan unalengwa mara kwa mara na wanamgambo wa Kiislamu walio na itikadi kali, sambamba na makundi ya wale wanaotaka kujitenga. Shambulio hilo linatokea huku kukiwa na ongezeko la ghasia baada ya kuvunjika kwa mazungumzo ya amani kati ya Islamabad na wanamgambo wa Taliban waliojificha nchini Afghanistan. Kundi la Taliban la Pakistan limeua takriban watu elfu  80,000 katika miongo kadhaa ya vurugu.