1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanajeshi 19 wa Ukraine wauwawa kwenye shambulio la Urusi

6 Novemba 2023

Ukraine imethibitisha kwamba wanajeshi wake 19 wameuwawa katika shambulio la makombora la Urusi lililofanywa katika mji wa Zaporizhizhia wakati wa sherehe ya kuwatunukia tuzo wanajeshi.

https://p.dw.com/p/4YTeu
Askari jeshi wa Ukraine akiwa katika uwanja wa vita
Askari jeshi wa Ukraine akiwa katika uwanja wa vitaPicha: Ozge Elif Kizil/Anadolu/picture alliance

Rais Volodymyr Zelensky amesisitiza kwamba tukio hilo la mauaji lingeweza kuepukika .

Waziri wa ulinzi Rustem Umerov ametoa maagizo ya kufanyika uchunguzi kuhusu tukio hilo kubaini kwanini brigadia maalum ya jeshi la operesheni za milimani ilishiriki katika sherehe hiyo iliyohudhuriwa na watu wengi Ijumaa iliyopita.

Soma pia:Zelensky hayuko tayari kuzungumza na Urusi

Tangazo hilo limekuja wakati maafisa wakiripoti kutokea  mashambulizi yaliyofanywa na ndege isiyokuwa na rubani ya Urusi pamoja na makombora na kujeruhi  watu wanane  na kuharibu jengo la makumbusho ya sanaa ambayo ni  sehemu ya  turathi za dunia zilizoorodheshwa na shirika la Elimu Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO.

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW