1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaijeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa magavana

Angela Mdungu
18 Machi 2023

Mamilioni ya Wanaijeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa magavana, ikiwa tayari umepita mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa Rais ulioshuhudiwa na changamoto kadhaa, ikiwemo teknolojia.

https://p.dw.com/p/4OsY2
Nigeria | Wahltag
Picha: Uwais Abubakar Idris/DW

Mamilioni ya Wanaijeria wanapiga kura leo katika uchaguzi wa magavana, mwezi mmoja baada ya uchaguzi wa Rais wa mwezi uliopita.

Uchaguzi huo utafanyika katika majimbo 28 kati ya majimbo 36 nchini humo wakati vyama vya upinzani vikiendelea kupinga ushindi wa Rais mteule Bola Tinubu. Jana Ijumaa, vikosi vya usalama vilionekana vikifanya doria katika mitaa ya majimbo yatakayofanya uchaguzi.

Licha ya hilo, muungano wa makundi ya asasi za kiraia umetoa kauli kuhusu hali ya usalama ilivyo na kudai kuwa uchaguzi huo wa magavana unafanyika kukiwa na mivutano, utekaji nyara na mauaji katika majimbo kadhaa.

Soma pia:Wanigeria waandamana kupinga matokeo ya uchaguzi

Mapema wiki hii, mshauri wa masuala ya usalama wa NigeriaBabagana Monguno, alisema vikosi vya usalama vimepelekwa katika maeneo yote hatari kwa vurugu na hawatazamii tukio lolote kubwa la kutishia amani.