1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na Haki

Wanaharakati wakosoa kukamatwa kwa Bobi Wine

21 Agosti 2018

Uganda imekumbwa na vurugu kwa takriban wiki moja sasa kufuatia hatua ya serikali kuwashikilia wabunge wawili, mmoja wao akiwa mkosoaji mkubwa wa rais Yoweri Museveni na ambaye pia ni msanii, Bobi Wine.

https://p.dw.com/p/33Spm
Robert Kyagulanyi Ssentamu aka Bobi Wine
Picha: Getty Images/AFP/Stringer

J2:21.08.2018- Interview on Uganda updates - MP3-Stereo

Kwa mujibu wa ripoti, wabunge hao wako katika hali inayotia hofu baada ya kupigwa. Waandamanaji ambao wamekuwa wakijitokeza pia wamekabiliwa na nguvu za vyombo vya dola  na mtu mmoja aliuawa kwa kupigwa risasi. Je, watetezi wa haki za binaadamu katika mataifa jirani wanayaangalia vipi matukio hayo ?John Juma amezungumza na mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za binadamu "Article 19" Afrika Mashariki, Henry Maina akiwa Nairobi Kenya, na kwanza anaelezea juu ya mtizamo wake kuhusu kile kinachotokea nchini Uganda.