1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati wa mazingira kuendeleza maandamano leo

Sylvia Mwehozi
16 Septemba 2023

Maelfu ya wanaharakati wa mazingira duniani kote leo wanatarajiwa kuendeleza maandamano yaliyoanza jana.Maandamano hayo yanalenga kuzishinikiza serikali duniani kuondokana na matumizi ya nishati ya kisukuku.

https://p.dw.com/p/4WPWy
Deutschland Globale Proteste von "Friday for future"
Picha: Markus Schreiber/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Maelfu ya wanaharakati wa mazingira duniani kote leo wanatarajiwa kuendeleza maandamano yaliyoanza jana kushinikiza viongozi wa dunia kuchukua hatua za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.

Maandamano hayo yanalenga kuzishinikiza serikali duniani kuondokana na matumizi ya nishati ya kisukuku hasa wakati huu ambapo dunia inakabiliwa na majanga ya kiasili na ongezeko la joto.

Maandamano hayo, yaliyopangwa na mashirika ya kikanda na kimataifa ya mazingira likiwemo vuguvugu la mwanaharakati kijana Greta Thunberg la Friday for Future, yanafanyika katika nchi 50 na miji mbalimbali duniani na yataendelea hadi siku ya Jumapili.

Wiki iliyopita, Umoja wa Mataifa ulionya kuwa mataifa bado yako nyuma kufikia lengo la kupunguza ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celcius, kulingana na malengo ya mkataba wa mazingira wa Paris wa mwaka.