1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanaharakati Uganda wakerwa na hatua ya kukamatwa Sewanyana

24 Septemba 2021

Wanasiasa wa upinzani nchini Uganda wameshtumu kitendo cha kukamatwa tena mbunge Allan Sewanyana kwenye lango la gereza mara tu baada ya kuachiwa kwa dhamana.

https://p.dw.com/p/40oHY
Uganda Bobi Wine
Picha: Ronald Kabuubi/AP Photo/picture alliance

Kulingana na walioshuhudia tukio hilo watu wanaoaminika kuwa maafisa wa vyombo vya usalama waliokuwa na bunduki walimvizia bwana huyo ghafla baada ya  kutoka kwenye gereza.

Walimtia katika gari moja ya kiraia na kutoweka naye.

Rais wa chama cha NUP Robert Kyagulanyi pamoja na kiongozi wa upinzani Dkt Kizza Besigye wamekitaja kitendo hicho kuwa ushahidi unaoonyesha utawala hauheshimu maamuzi na maagizo ya mahakama,wakati pia wakisema kisa hicho ni miongoni mwa visa vingi vya utekaji nyara vinavyoshuhudiwa kila mara.

Msemaji wa magereza Frank Baine ameoindolea lawama taasisi yake akisema, walitimiza wajibu wao kwa mujibu wa maagizo ya Mahakama na hawahusiki hata kidogo na kile kilichotokea.

Lakini hatimaye msemaji wa majeshi Brigedia Flavia Byekwaso amesambaza  taarifa akisema mbunge huyo alikamatwa kuhusiana na madai mapya ya wanasiasa wa chama chake kuvunja sheria.