1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliokufa kutokana na maporomoko wafikia 68 Tanzania

5 Desemba 2023

Idadi ya waliofariki katika maporomoko ya udongo kufuatia mvua kubwa iliyonyesha nchini Tanzania imefikia watu 68 huku wengine 116 wakiripotiwa kujeruhiwa.

https://p.dw.com/p/4Zmih
Tansania Erdrutsch Katesh
Picha: Xinhua/picture alliance

Hayo yameelezwa na Queen Sendiga, mkuu wa mkoa wa Manyara uliokumbwa na maafa hayo. Kikosi cha wataalam wapatao 350 kutoka jeshini kimetumwa eneo hilo kusaidia zoezi la uokozi. Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alitangaza kuwa serikali itagharamia mazishi ya waathiriwa.Mvua kubwa ilinyesha siku ya Jumamosi jioni na kusababisha maporomoko ya udongo kwenye mlima Hanang. Mji wa Katesh, ulio chini ya mlima huo uliathiriwa pakubwa. Nchi nyingi za Afrika Mashariki zimekuwa zikikumbwa kwa wiki kadhaa na mvua kubwa na mafuriko yanayohusishwa na El Niño.