1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Waliokufa jkwa tetemeko Uturuki wafikia 50,800

22 Aprili 2023

Kulingana na takwimu za serikali ya Uturuki, idadi ya watu waliofariki katika maafa ya matetemeko makubwa mawili ya ardhi mnamo mwezi Februari imeongezeka na kufikia watu 50,782

https://p.dw.com/p/4QRQg
Türkei Syrien Erdbeben Antakya
Picha: Hussein Malla/AP Photo/picture alliance

Kulingana na takwimu za serikali ya Uturuki, idadi ya watu waliofariki katika maafa ya matetemeko makubwa mawili ya ardhi mnamo mwezi Februari imeongezeka na kufikia watu 50,782.Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uturuki Süleyman Soylu amesema miongoni mwa watu waliokufa walikuwemo wageni wapatao 7,300. Februari 6, matetemeko mawili ya nguvu yenye ukubwa wa 7.7 na 7.6 katika kipimo cha Richta yalitikisa kusini-mashariki mwa Uturuki na kaskazini mwa Syria. Zaidi ya watu milioni 2 walipoteza makazi yao nchini Uturuki.Wiki iliyopita, dhoruba ilipiga katika eneo lililokumbwa na tetemeko la ardhi nchini Uturuki ambapo mtu mmoja alifariki na wengine 50 walijeruhiwa. Dhoruba hiyo pia ilisababisha uharibuifu wa mahema yanayowahifadhi watu walionusurika kwenye maafa ya mitetetemeko ya ardhi.