1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waliojaribu mapinduzi Sudan wafungamanishwa na Al-Bashir

21 Septemba 2021

Serikali ya Sudan imesema maafisa wa kijeshi na kiraia wanaohusika na utawala wa zamani ulioondolewa madarakani wa kiongozi wa zamani Omar Al Bashir ndio waliojaribu kufanya mapinduzi lakini walidhibitiwa bila vurugu.

https://p.dw.com/p/40c2b
Sudan | Ansprache Informationsminister Hamza Baloul nach Putschversuch
Picha: Sudan TV/AFP

Waziri wa habari Hamza Baloul amesema wamefanikiwa kudhibiti jaribio la mapinduzi la maafisa wa kijeshi asubuhi ya Jumanne.

Kwa mujibu wa waziri huyo viongozi wa mapinduzi hayo wamekamatwa.

Vikosi vya usalama inaarifiwa kwamba vimelifunga daraja kuu la kupita Mto Nile linalouunganisha mji wa Khartoum kwenda mji wa Omdurman.

Sudan inaongozwa na serikali ya mpito iliyopatikana baada ya kuondolewa kwa nguvu madarakani rais wa zamani Omar al Bashir, serikali ambayo inawajumuisha wajumbe wa kijeshi na kiraia.