1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNiger

Wakuu wa majeshi ECOWAS wakutana kuijadili Niger

17 Agosti 2023

Wakuu wa majeshi wa mataifa ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS, wanakutana katika mji mkuu wa Ghana, Accra kujadili uwezekano wa kuingilia kati kijeshi nchini Niger.

https://p.dw.com/p/4VGyt
Nigeria  Abuja | ECOWAS Treffen Verteidigungsminister
Picha: Chinedu Asadu/AP Photo/picture alliance

Hata hivyo wanajeshi waliotwaa madaraka wamesema wapo tayari kwa mazungumzo lakini bado wanamshilikia rais waliyempindua, Mohammed Bazoum na wamesema watamfungulia mashtaka ya uhaini.

Soma pia:Wanajeshi 17 wa Niger wauawa katika shambulizi karibu na Mali

Kujiingiza kijeshi kwa namna yoyote, utaliyumbisha zaidi eneo masikini la Sahel ambapo makundi ya kigaidi yanayohusiana na mtandao wa magaidi wa al Qaeda pamoja na kundi linaloitwa dola la kiislamu yameleta vurumai na kusababisha mamilioni ya watu wageuke wakimbizi wa ndani.

Mnamo kipindi cha miaka 10 iliyopita vurumai za makundi hayo zimesababisha njaa kwenye eneo la Sahel.