1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa Rohingya waandamana kupinga hali duni ya maisha

31 Mei 2021

Polisi nchini Bangladesh inasema maelfu ya Warohingya wameandamana leo kupinga hali duni ya maisha katika kisiwa kimoja ambacho hupigwa na vimbunga vya mara kwa mara.

https://p.dw.com/p/3uEI6
Bangladesch Rohingya Flüchtlinge Cox’s Bazar | Protest gegen Rückführung
Picha: picture-alliance/AP Photo/D. Yasin

Kulingana na polisi karibu watu 4000 wameshiriki maandamano hayo na yamefanyika wakati ambapo kulikuwa na ziara ya maafisa wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR.

Mtu mmoja wa kabila la Rohingya ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP kuwa waandamanaji wamerusha mawe na polisi waliwazuia kuingia katika jengo ambamo maafisa wa UNHCR walikuwemo.

soma zaidi: Kundi la kwanza la wakimbizi wa Rohingya lawasili kisiwa cha Bangladesh

Tangu Desemba, Bangladesh imewahamisha wakimbizi 18,000 na kuwapeleka katika kisiwa hicho cha Bhashan Char kilicho katika eneo la chini ambapo idadi jumla ya watu 850,000 wanaishi katika hali duni.

Bangladesh inapania kuwahamisha wakimbizi laki moja na kuwapeleka katika kisiwa hicho.