1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wakimbizi wa Eritrea warudi kwa hiari nyumbani:

14 Novemba 2003
https://p.dw.com/p/CEDc
TESENEY,ERITREA: Kiasi wakimbizi elfu moja wa Eritrea wakiandamana na mkuu wa Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa, Ruud Lubbers, walivuka mpaka wa Sudan jana, wakirudi nyumbani kwa hiari zao, kutokana na chanzo cha Umoja wa Mataifa. Waziri mkuu huyo wa zamani wa Uhollanzi, Lubbers, alisema bado kuna wakimbizi wengi wa Eritrea nchini Sudan, na ameridhika jinsi utaratibu wa kuwarudisha nyumbani unavyoendelea. Kurudi nyumbani wakimbizi hao, ni sehemu ya makubaliano ya amani. Hadi kati kati ya miaka 80, Wa-Eritrea nusu millioni wamekuwa wakiishi Sudan na wengi waliondoka baada ya nchi yao kuunganishwa na Ethiopia, na hayati mfalme Haile Selassie mwaka 1962.