1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Mtindo wa maishaKenya

Wakenya wageukia dawa za kiasili na kuacha za hospitalini

Shisia Wasilwa
17 Julai 2024

Wimbi la madadiliko linazidi kupepea nchini Kenya, na kila linapopita linaleta athari chanya, likibadilisha mawazo ya wakenya wengi wanaokumbatia dawa za kiasili na kuachana na dawa za hospitalini. Shisia Wasilwa anakufahamisha ni kwanini hilo linashuhudiwa nchini humo.

https://p.dw.com/p/4iPTH

Wimbi la mabadiliko linazidi kupepea nchini Kenya na linabadilisha mawazo ya Wakenya wengi kugeukia dawa za kiasili na kuacha dawa za hospitalini. Wanaobadilishwa mawazo wanadai kuwa dawa za asili hazina madhara yoyote zikilinganishwa na dawa za hospitalini. Katika Makala ya Wanawake na Maendeleo leo Shisia Wasilwa anamwangazia mama Abigael Chebet anayeuza dawa za kiasili katika jimbo la Baringo nchini Kenya.