1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiBurundi

Wake wa viongozi Afrika himizeni ajenda ya uzazi wa mpango

9 Oktoba 2023

Ongezeko la idadi ya watu limetajwa kuwa na athari kuanzia ngazi ya familia na nchi kwa ujumla wake, hivyo wito kwa wake wa viongozi umetolewa kuhakikisha ajenda ya uzazi wa mpango inasonga mbele.

https://p.dw.com/p/4XJfW
Marium Mwinyi mke wa Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi akizungumza na mwandishi wa habari wa DW Salma Said
Marium Mwinyi mke wa Rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi akizungumza na mwandishi wa habari wa DW Salma SaidPicha: Salma Said/DW

 Amesema hayo Angeline Ndayishimiye mke wa rais wa Burundi kwenye kongamano la 4 la wanawake viongozi lilizinduliwa Bujumbura.

Kongamano hilo la limehuudhuriwa na wake wa marais wa Kenya, Rwanda, Zanzibar na wale kutoka matawi mbali mbali ya Umoja wa Mataifa. 

Wanawake viongozi wanalo jukumu la kuhakikisha uzazi wa mpango katika jamii, njia itakayoruhusu lishe bora na kufikia maendeleo endelevu, ni kauli mbiu hiyo inayojadiliwa katika mkutano huo ulozinduliwa hapa Bujumbura.

Soma pia:Mpango wa uzazi kwa njia ya homoni huongeza hatari ya saratani ya matiti

Mkutano huo uloandaliwa na kituo OPDD kinachoongozwa na mke wa rais, Bi amesema dhamira ya mkutano huo ni kukabiliana na ongzeko la watu kwani limekuwa likiathiri maenddeleo yanayokusudiwa.

"Tunatakiwa kuepuka uzazi pasina mpango, kwani hupelekea afya ya mwanamke kuzorota,"

Ameongeza kuwa watoto hulelewa bila uangalizi unaohitajika kwa makuzi ya watoto, huku mama akishindwa kujihusisha na shughuli za maendeleo ya jamii na hata ya nchi.

Mwanamke anabeba mtoto mmoja mgongoni, mwingine kwenye mapaja,
na mwingine akiwa tumboni. Magonjwa ya utapiamlo, kipato kinakuwa hafifu, ugomvi katika familia, huku migogoro ya ardhi ikifuatia. Alisema mke wa rais Angeline Ndayishimiye.                                                                                         

Uzazi wa mpango unalinda afya ya jamii            

Kwa upande wake Bi Mariam Mwinyi, mke wa rais wa Zanzibar, amesema uzazi wa mpango unasaidia pia kupunguza vifo vya uzazi kwa zaidi ya asilimia
30.

Vijana hupendelea njia zipi za uzazi wa mpango?

Na kwamba Tanzaniabara kuna asilimia 81 ya wanawake wanaojifungua katika  vituo vya afya na asilimia 86 kwa Zanzibar.

Soma pia:Utumiaji holela wa vidonge vya uzazi vya P2 kwa wasichana na hatari inayowakabili

Swala la uzazi wa mpango na lishe bora lazima liorodheshwe katika miradi mikuu ya serikali, kwa kubuni sera na mikakati inayofaa.

Alisema Abdoul Dieng, mwakilishi mkaazi wa  mashirika ya Umoja wa Mataifa Burundi.

Mkutano huo wafuatia mwingine wa aina hii ulofanyika mwenye Oktoba mwaka jana ambapo wanawake viongoziwalitakiwa  kuzidisha juhidi ili kuboresha afya na licha ya mama na mtoto na vijana baleghe.