1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Wahouthi washambulia meli nje ya pwani ya Kusini mwa Yemen

12 Februari 2024

Mashirika ya usalama wa majini, yamesema meli moja imekabiliwa na mashambulizi katika pwani ya Kusini mwa Yemen leo Jumatatu wakati ikipita katika eneo la kimkakati la mlango bahari la Bab al-Mandeb.

https://p.dw.com/p/4cIUR
Mzozo wa Mashariki ya Kati -Mashambulizi dhidi ya Meli Bahari ya Shamu
Meli ikiwaka moto baada ya kushambuliwa na WahouthiPicha: Indian Navy/AP/dpa/picture alliance

Shirika la shughuli za usafiri wa majini la Uingereza UKMTO limesema tukio hilo limetokea alfajiri na wafanyakazi wa meli hiyo wameripotiwa kuwa salama wakati meli hiyo ikiendelea na safari yake kuelekea kwenye bandari nyingine.

Shirika jingine la masuala ya usalama la Ambrey limesema meli hiyo iliyokuwa ikipeperusha bendera ya Jamhuri ya visiwa vya Marshall  na inayomilikiwa na kampuni moja ya Ugiriki ililengwa kwa makombora katika matukio mawili tofauti ndani ya kipindi cha dakika 20.

Soma pia: Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wazidisha mashambulizi katika Bahari ya Shamu

Mmiliki wa meli hiyo ni miongoni mwa walioko kwenye soko la hisa la Marekani NASDAQ. Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakizilenga meli zinazipita katika bahari ya Sham tangu mwezi Novemba na kusababisha mashambulizi ya kupiza kisasi ya Uingereza na Marekani.

 

DW Kiswahili | Saumu Mwasimba
Saumu Mwasimba Mhariri na mtangazaji wa Idhaa ya Kiswahili ya DW