1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahouthi waizamisha meli ya mizigo Bahari ya Shamu

19 Juni 2024

Meli moja ya mizigo imezama katika Bahari ya Shamu baada ya shambulizi baya lililofanywa na waasi wa Yemen wiki iliyopita kuipelekea meli hiyo kuachwa baharini.

https://p.dw.com/p/4hEg6
Operesheni ya Wahouthi dhidi ya meli zenye mafungamano na Israel kwenye Bahari ya Shamu.
Operesheni ya Wahouthi dhidi ya meli zenye mafungamano na Israel kwenye Bahari ya Shamu.Picha: Mohammed Hamoud/picture-alliance

Kulingana na Shirika la Operesheni za Baharini la Uingereza (UKMTO), meli hiyo ya MV Tutor iliyokuwa na bendera ya Liberia na inayomilikiwa Ugiriki, ililengwa na droni kutoka baharini katika eneo la Hodeida mnamo Juni 12.

Meli hiyo ni ya pili kuzamishwa na Wahouthi katika miezi ya hivi karibuni baada ya meli ya Rubymar, ambayo ilikuwa imebeba maelfu ya tani ya mbolea.

Soma zaidi: Wafanyakazi tisa wa UN washikiliwa na Waasi wakihouthi Yemen

Meli hiyo ilizama katika Bahari ya Shamu mnamo mwezi Machi baada ya shambulizi la kombora.

Waasi wa Kihouthi wamekuwa wakifanya mashambulizi ya droni na makombora katika njia muhimu ya Bahari ya Shamu tangu mwezi Novemba, wakisema  wanalipiza kisasi kwa vita vya Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza.