1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahariri wa magazeti walizungumzia sakata la kashfa ya unasaji wa simu za faragha

Abdu Said Mtullya20 Julai 2011

Uingereza bado yasakamwa na kashfa ya magazeti.

https://p.dw.com/p/120D3
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron.Picha: dapd

Karika maoni yao leo wahariri wa magazeti ya hapa nchini wanazungumzia juu ya kashfa ya udakizaji wa simu nchini Uingireza.

Mmiliki maarufu wa vyombo vya habari Rupert Murdoch jana alitolewa jasho na wabunge wa Uingereza walipomhoji juu ya kasha ya kuzidakiza simu za watu iliyolihusisha gazeti lake la News Of The World .

Juu ya mkabala wa jana baina ya Murdoch na wabunge wa Uingereza gazeti la Stuttgarter linasema hadhi ya Murdoch, mfalme wa tasnia ya vyombo ya habari , iliteremka mbele ya wabunge wa Uingereza. Hadi hivi karibuni tu Murdoch alikuwa anaamua ni nani alietaka kukutana naye ofisini mwake. Lakini jana dunia ilipinduka kichwa chini -miguu juu kwa bwana Murdoch.

Mhariri wa gazeti la Main Echo anawasuta wasomaji wa magazeti nchini Uingereza kuhusiana na kashfa ya udakizaji wa simu. Anasema thama na wao, watu kama Murdoch na wenzake wasingelifanikiwa . Mhariri huyo anaeleza kuwa Murdoch na wenzake wamefanikiwa kwa sababu wasomaji wanataka kujua juu ya mambo ya kusisimua. Kwa hiyo sasa wale wanaojaribu kuwashutumu Murdoch na wenzake wanapaswa kujiuliza iwapo wao pia hawakuchangia, katika kashfa iliyotokea ,kutokana na kulinunua gazeti la News Of the World.

Gazeti la Nürnberger Nachrichten linatilia maanani kwamba ni waandishi wa habari waadilifu walioifichua kashfa ya udakizaji wa simu za faragha Hayo yanathibitisha kwamba, vyombo vya habari nchini Uingereza bado vinao uwezo wa kuiepusha Uingereza kugeuka jamhuri ya Anchuria yaani nchi inayotawaliwa na dikteta.

Gazeti la Delmenhorster Kreisblatt linasema habari juu ya kashfa ya unasaji wa simu za faragha ni za kushtusha sana ,lakini ni jambo la kutia moyo kwamba kashfa kama hiyo ni jambo lisilowezekana nchini Ujerumani.

Hatahivyo mhariri huyo anatahadharisha
kwamba watu mashuhuri nchini Ujerumani aghalabu huhisi kuwa wanaandamwa na waandishi wa habari. Ndugu wa watu waliokumbwa na matukio ya ajali pia wanabughudhiwa na waandishi wa habari. Polisi wanapofanya misako, tayari kamera zinakuwapo. Waandishi habari wanajuaje? Waandishi hao wanapata habari za uhakika kutoka Polisi- jee hiyo ni nasibu? Hakika mambo hayo hayawezi kutokea kwa nasibu.

Mwandishi/Mtullya abdu/Deutsche Zeitungen /

Mhariri/- Abdul -Rahman.