1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji wapatao 1000 wakamatwa pwani ya Libya

30 Machi 2021

Walinzi wa pwani ya Libya wamewakamata kiasi cha wahamiaji 1000 ndani ya kipindi cha siku mbili katika eneo lake la pwani ya magharibi mwa nchi hiyo waliokuwa wakijaribu kuelekea Ulaya.

https://p.dw.com/p/3rNTp
Mittelmeer Libyen | NGO Open Arms hilft Migranten im Holzboot
Picha: Joan Mateu/AP/picture alliance

Hayo yameelezwa na shirika la kimataifa la kusghulikia wahamiaji IOM. Ofisi ya shirika hilo nchini Libya imesema katika kipindi cha zaidi ya saa 48 takriban wahamiaji 1000 walizuiwa na kukamatwa na kurudishwa nchini Libya na walinzi wa pwani pamoja na kikosi cha usalama wa pwani ya nchi hiyo.  

Safa Msehli ambaye ni msemaji wa shirika hilo la Umoja wa Mataifa lenye makao yake mjini Geneva Uswizi amesema kupitia ujumbe wa Twitta kwamba waliokamatwa ni pamoja na watoto wanawake na wanaume.

soma zaidi:

Kadhalika shirika hilo limeonya kwamba wahamiaji huenda wakakabiliwa na hatua ya kuwekwa kizuizini.

Nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ni njia kubwa ya wahamiaji wanaojaribu kuelekea Ulaya kupitia bahari ya Mediterrania na wasafirishaji binadamu kwa njia za magendo wanatumia fursa ya ukosefu wa uthabiti, kufuatia kuangushwa utawala wa aliyekuwa kiongozi wa nchi hiyo Moammar Kadhafi, kuimarisha shughuli zao.