1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wahamiaji 89 wafa maji Mauritania

5 Julai 2024

Wahamiaji wapatao 90 waliokuwa wakielekea Ulaya wameghariki na wengine kadhaa hawajuilikani walipo baada ya mashua yao kupinduka kwenye bahari ya Mauritania.

https://p.dw.com/p/4htDj
Mauritania
Wahamiaji kwenye boti ya wavuvi Mauritania.Picha: Annika Hammerschlag/AA/picture alliance

Shirika la habari la nchi yao limesema kwamba walinzi wa pwani wameipowa miili 89 waliokuwa kwenye mashua kubwa ya uvuvi kwenye ufukwe wa Bahari ya Atlantiki, umbali wa kilomita nne kutoka mji wa kusini magharibi wa Ndiago.

Walinzi hao walifanikiwa kuwaokowa watu wengine tisa wakiwa hai, akiwemo msichana wa miaka mitano.

Soma zaidi: Wahamiaji 11 wafa baharini, 60 hawajulikani waliko

Kwa mujibu wa manusura, mashua hiyo ilikuwa inatokea mpaka wa Senegal na Gambia ikiwa na abiria 170 ndani yake, hiyo ikimaanisha kuwa watu ambao hawajaonekana ni zaidi ya 70.

Ingawa njia ya kutumia Bahari ya Atlantiki ni mbaya zaidi kutokana na mkondo mkali wa maji, lakini watu wanaojaribu kuingia barani Ulaya wamekuwa wakiitumia badala ya Bahari ya Mediterenia yenye ulinzi mkali.